Chakula
Chakula hulisha miili na akili zetu na kutuunganisha na utamaduni na jamii yetu. Ikiwa pesa hazitoshi, wakati wa chakula unaweza kuwa chanzo cha mfadhaiko. Kuna chaguzi nyingi hapa Maine za kusaidia wewe na familia yako kupata chakula.
Be There for ME ni ya wazazi na watunzji wote katika Maine, na watu wanaowasaidia. Kupata msaada kunaweza kuwa jambo ngumu na huchukua muda. Chukua hatua ya kwanza leo, hata kama hujui uende wapi. Rasilimali zilizoko kwenye tovuti ni mahali pasipo kuhukumiwa pa kuanza kutafuta msaada.