Hisia au Mfadhaiko wa Mtoto Wangu

Furaha, hasira, msisimko, huzuni. Kama vile inaweza kuwa ngumu kudhibiti hisia na mfadhaiko wako, inaweza kuwa ngumu kusaidia mtoto wako na hisia zake. Kuanzia vikundi rika na simu za dharura hadi watabibu, kuna msaada hapa Maine kwa ajili yako na mtoto wako. 

Nahitaji msaada kwa mtoto wangu sasa hivi

988 National Suicide & Crisis Lifeline

na 988

Mambo yakizidi, wewe au mtoto wako mnaweza kupiga simu, kutuma ujumbe, au kupiga gumzo ili kupata msaada wa siri 24/7. Kutakuwa na mtu upande ule mwingine atakayekusikiliza na kuzungumza nawe. 

Image
988 lifeline logo

Nataka kuzungumza na mtu ambaye anaweza kunisaidia kuelewa

Daktari wa mtoto wako, muuguzi wa shule, au mfanyakazi wa kijamii wa shule

Daktari wa mtoto wako, muuguzi wa shule, au mfanyakazi wa kijamii wa shule anaweza kutambua misaada kwa mtoto wako na jinsi ya kuipata.

Image
Yellow badge with Childs head outlined with brain outline in middle

G.E.A.R. Parent Network

Unaweza kuzungumza na wazazi wengine ambao wamepitia jambo hilo na kupata habari kuhusu msaada. 

Image
GEAR Parent Network Logo

Nataka kuzungumza na mtu ambaye anaelewa

Nataka kujua kuhusu misaada ambayo naweza kushiriki na mtoto wangu

NAMI Maine Teen Text Line

(207) 515-8398 

Ikiwa mtoto wako ana umri wa miaka 13-23, anaweza kutuma ujumbe mfupi wa siri kwa simu hii ya msaada. Mtaalamu wa msaada aliyehitimu mwenye umri wa miaka 18-24 atajibu wakati wa masaa ya kazi.

Image
NAMI Maine Logo

Nataka kujua kuna nini kingine huko nje

Be There for ME ni ya wazazi na watunzaji wote kule Maine, na watu wanaowasaidia. Kupata msaada kunaweza kuwa jambo ngumu na huchukua muda. Chukua hatua ya kwanza leo, hata kama hujui uende wapi. Rasilimali zilizoko kwenye tovuti hii ni mahali pasipo na kuhukumiwa pa kuanza kutafuta msaada.

Father speaking with his children