Afya au Maendeleo ya Mtoto Wangu
Kama mzazi au mtunzaji, hakuna furaha kubwa kuliko kuona mtoto wako akikua na kujifunza. Kila mtoto ni tofauti, na mahitaji yake pia ni tofauti kadiri anavyoendelea kukua. Inaweza kuwa ngumu kwa mzazi kujua kile ambacho mtoto wako anahitaji, wakati anapokihitaji, na mahali pa kukipata. Msaada upo kwa ajili yako na mtoto wako katika safari hii.
Be There for ME ni ya wazazi na watunzaji wote kule Maine, na watu wanaowasaidia. Kupata msaada kunaweza kuwa jambo ngumu na huchukua muda. Chukua hatua ya kwanza leo, hata kama hujui uende wapi. Rasilimali zilizoko kwenye tovuti hii ni mahali pasipo na kuhukumiwa pa kuanza kutafuta msaada.