Hisia Zangu au Mfadhaiko

Maisha yanaweza kuleta furaha kubwa na pia changamoto kubwa - kama vile uzazi. Kila mtu ana nyakati za kuhisi kama amezidiwa na mambo. Kuzungumza na rafiki, tabibu, au kikundi cha utegemezo kwaweza kuleta tofauti kubwa. Kuna msaada hapa Maine wa kukusaidia kukabilina na nyakati hizo ngumu kama mtu binafsi - na kama mzazi au mtunzaji.  

Angalia ukurasa huu ikiwa unatafuta usaidizi wa dawa za kulevya au pombe.

Ninahitaji msaada sasa hivi

988 National Suicide & Crisis Lifeline

na 988

Ikiwa unahisi kama mambo yamezidi, unaweza kupiga simu, kutuma ujumbe, au kupiga gumzo ili kupata msaada wa siri 24/7. Mtu atakuwa upande ule mwingine ili kukusikiliza na kuzungumza nawe. 

Image
988 lifeline logo

Nataka kuzungumza na mtu ambaye anaelewa

Maine's Peer Support Warmline

1-866-771-WARM (9276)

Ikiwa unataka kuzungumza na mtu ambaye amepitia jambo kama hili, unaweza kupiga simu nambari hii 24/7. 

Image
Maine Peer Support Line logo

Nataka kujifunza kuhusu njia za kukabiliana nalo

Strengthen ME

Unaweza kupata njia za kukabiliana na mfadhaiko na kujifunza kuhusu misaada ya ustawi katika jimbo lote.

Image
Strengthen ME logo

NAMI Maine Respite Care

Ikiwa wewe ni mzazi au mtunzaji wa mtoto mwenye mahitaji makubwa, mapumziko yanaweza kukusaidia kupata muda wa kujitunza. 

Image
NAMI Maine Logo

Nataka kujua kuna nini kingine huko nje

Be There for ME ni ya wazazi na watunzaji wote kule Maine, na watu wanaowasaidia. Kupata msaada kunaweza kuwa jambo ngumu na huchukua muda. Chukua hatua ya kwanza leo, hata kama hujui uende wapi. Rasilimali zilizoko kwenye tovuti hii ni mahali pasipo na kuhukumiwa pa kuanza kutafuta msaada.

A stressed out mother