Kupata Vitu vya Kila Siku

Kuendesha familia kunahitaji vitu vingi! Vitu ambavyo wewe na watoto wako mnahitaji vinaweza kukulemea kiakili na kifedha. Huenda kuna msaada hapa Maine wa kupata kile unachohitaji, iwe ni nepi, nguo, au kitu kingine.

Angalia kurasa hizi ikiwa unatafuta msaada wa chakula au usafiri
 

Nataka mtu anisaidie kupata kile ninachohitaji

Community Action Agencies

Kuna shirika la jamii la utekelezaji katika kila kaunti Wafanyakazi wa shirika hilo wanaweza kusaidia kukuunganisha kwa chochote unachohitaji ili ufike unapohitaji kwenda, na msaada mwingine pia.

Image
MeCAP logo

Community Care Program

Unaweza kuunganishwa na mtu ili kuzungumza kuhusu unachotafuta, kwa kuzingatia mahitaji yako ya kitamaduni na ya lugha.

Image
OPHE logo

Help Me Grow Maine

Ikiwa una mtoto mwenye umri wa miaka 8 au chini, unaweza kuzungumza na mtaalamu wa msaada wa familia. Anaweza kusaidia kupata rasilimali za jamii ambazo zinaweza kukidhi mahitaji yako na kupendekeza msaada mwingine. 

Image
help me grow maine logo

Ninahitaji msaada kulipia kitu sasa hivi

General Assistance

Unaweza kupata msaada kutoka kwa mji au jiji lako ili kukusaidia kulipia mahitaji ya kimsingi, ikiwa ni pamoja na kodi, mafuta na huduma zingine na vifaa vya nyumbani.

Image
A circular yellow badge with a simple house symbol in the center.

Nataka kujua kuna nini kingine huko nje

Be There for ME ni ya wazazi na watunzji wote katika Maine, na watu wanaowasaidia. Kupata msaada kunaweza kuwa jambo ngumu na huchukua muda. Chukua hatua ya kwanza leo, hata kama hujui uende wapi. Rasilimali zilizoko kwenye tovuti ni mahali pasipo kuhukumiwa pa kuanza kutafuta msaada.

Mother and daughter tourists buying clothes on local street market in Cinque Terre, Spain.