Be There for ME

Kusaidia Wazazi na Watunzaji kule Maine

Inaweza kuwa vigumu kuomba msaada au hata kujua kuna nini huko nje. Hauko peke yako. Be There for ME ni mahali pa kuanza kupata msaada.

Maisha yanapokuwa magumu (na huwa hivyo) msaada uko kule nje.

Kujitunza na kuwatunza watoto wako kunaweza kuwa jambo gumu. Ingawa watoto huleta furaha kubwa, kuwa mzazi sio jambo rahisi kabisa. Kila mtu anahitaji msaada wakati mwingine, iwe ni kulipa bili, kupata huduma ya utunzaji wa watoto ya bei nafuu, au kushughulikia hisia na mafadhaiko yako mwenyewe. Be There for ME ni mahali pasipo na hukumu pa  kuunganishwa na msaada.

Happy Hispanic mother and son portrait
Woman with baby smiling

Nini maana ya Be There for ME?

Be There for ME ni ya wazazi na watunzaji wote kule Maine, na watu wanaowasaidia. Kupata msaada kunaweza kuwa jambo ngumu na huchukua muda. Chukua hatua ya kwanza leo, hata kama hujui uende wapi. Rasilimali zilizoko kwenye tovuti hii ni mahali pasipo kuhukumiwa pa  kuanza kutafuta msaada.

Kila mtu ana jukumu la kutimiza. Wewe si mzazi au mtunzaji? Unaweza kusaidia familia katika jamii yako kwa kushiriki Be There for ME na kutumia zana.

Be There for ME ilianzishwa na Department of Health and Human Services na Maine Child Welfare Action Network kwa ushirikiano na kikundi tofauti cha wazazi na watunzaji. Tovuti hii iliundwa kulingana na kile ambacho wazazi na walezi walisema wanahitaji na jinsi wanavyozungumza juu ya maisha yao. Rasilimali zilizoko kwenye wavuti hii sio orodha kamili ya misaada inayopatikana.