Dawa za Kulevya au Pombe

Ikiwa una wasiwasi kuhusu jinsi dawa za kulevya au pombe zinavyoathiri maisha yako, au maisha ya mtu unayempenda, msaada upo. Simulizi lako ni lako peke yako, lakini kuna watu ambao wanajua jinsi ilivyo vigumu kuomba usaidizi na wanataka kusaidia. 

Angalia ukurasa huu ikiwa unatafuta msaada wa hisia na mafadhaiko yako. 
Au ukurasa huu ikiwa unataka kusaidia kijana anayetumia dawa za kulevya au pombe.

Nataka kuzungumza na mtu ambaye anaelewa

OPTIONS Maine

Ikiwa unahitaji mtu wa kukusaidia kuelewa hatua yako inayofuata, unaweza kuwasiliana na mwakilishi wako wa jamii. Yeye husaidia watu kila siku na anaweza kukusaidia katika safari yako.

Image
Options Maine logo

Maine Recovery Hub

Ikiwa uko katika ahueni au unatafuta ahueni, unaweza kuunganishwa na kituo cha jamii au mkufunzi katika eneo lako. 

Image
PRCC logo

Maine QuitLink

Ikiwa unataka kusaidiwa kuacha kuvuta sigara, sigara za kielektroniki, au matumizi mengine ya tumbaku, kuna watu ambao wanaweza kukusaidia kujua hatua yako inayofuata.

Image
Maine QuitLink logo

Mimi ni mjamzito au mzazi mpya anayetafuta usaidizi

Maine MOM

Unaweza kuungana na timu ili kupata utunzaji unaohitaji na msaada unaposonga mbele.

Image
Maine MOM logo

Nataka kutafuta matibabu

Be There for ME ni ya wazazi na watunzji wote katika Maine, na watu wanaowasaidia. Kupata msaada kunaweza kuwa jambo ngumu na huchukua muda. Chukua hatua ya kwanza leo, hata kama hujui uende wapi. Rasilimali zilizoko kwenye tovuti ni mahali pasipo kuhukumiwa pa kuanza kutafuta msaada.

A pregnant woman with hand on her belly